loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Samia : Mradi wa mafuta utanufaisha pande mbili

RAIS  Samia Suluhu ameshuhudia utiaji saini wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani Tanzania (EACOP) ambapo amesema utafungua milango ya fursa kwa pande zote mbili.

Utiaji saini wa mkataba huo umeshuhudiwa pia na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda,  ambapo vipengele 56 vimefikiwa tayari kwa kuanza utekelezaji wa ujenzi huo utakaochukua miaka minne kukamilika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia alisema mradi huo wa bomba la mafuta utakuwa na faida kwa nchi zote mbili kwa kuongeza mapato na kutoa ajira kwa vijana, ambapo utasaidia  kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa nchi zote mbili.

“Mradi huu utakuwa na manufaa ya kiuchumi na kijamii, kwa pande zote mbili, utaongeza mapato kwa serikali zetu, na utatengeneza ajira za muda mfupi na mrefu, inakadiriwa zaidi ya ajira 10,000 zitapatikana,” amesema Rais Samia.

“Utakuza mahusiano ya kibiashara na kindugu kwa pande zote mbili, naamini mradi huu utakapokamilika utakuwa na faida kubwa si tu kwa Tanzania na Uganda bali kwa nchi zote za Afrika,”ameongeza.

Amesema awali mkataba huo ulikuwa usainiwe Machi 22, lakini kutokana na Tanzania kupatwa na msiba wa Hayati Rais Dk John Magufuli ambaye ana mchango mkubwa katika kufanikisha mradi huo, Uganda ilisitisha zoezi hilo.

“Makubaliano yanayofanyika leo yalitakiwa kufanyika Machi 22,  lakini baada ya kifo cha rais wetu John Magufuli mlisitisha (Rais Yower Museveni), hatua hiyo ilionyesha urafiki wa kweli, tunashukuru sana,” amesema.

Mwaka 2020, aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Museveni walisaini makubaliano ya jenzi wa bomba hilo unaogharimu dola za Marekani bilioni 3.5.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za Marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi