loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Real yaifunga Barca na kukaa kileleni

REAL Madrid imekaa kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kuifunga Barcelona kwa mabao 2-1 katika mchezo wa El Clasico uliopigwa, huku mvua ikinyesha kwenye Uwanja wa Alfredo Di Stefano.

Karim Benzema alifunga bao la kwanza kwa pasi ya nyuma likiwa bao lake la tisa katika mechi za La Liga dhidi ya wapinzani wao hao wakubwa.

Real Madrid walionesha makali yao pale walipofunga la pili kabla ya mapumziko kupitia kwa Toni Kroos aliyepiga mpira wa adhabu uliobadili mwelekeo na kujaa wavuni.

Oscar Mingueza alifungia Barcelona bao la kufutia machozi kabla Casemiro wa Real Madrid hajaoneshwa kadi nyekundu. Kiungo wa Barca Ilaix Moriba nusura aisawazishie timu yake baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba wakati wenyeji wakiendelea kuongoza.

Matokeo hayo yanaifanya Real Madrid kukaa juu ya wapinzani wao wa jiji, Atletico Madrid baada ya kushinda timu hizo zilipokutana. Atletico, ambayo ilikuwa ikiongoza kwa pointi 10 hivi karibuni, inaweza kukalia tena kiti hicho kama jana Jumapili itakuwa imeibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Real Betis.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa kwao kila mchezo ni sawa na fainali, huku wakipoteza pointi nne tu katika mechi walizocheza ugenini msimu huu

THOMAS Tuchel amesema Chelsea inakwenda fainali ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi