loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachimbaji wadogo waandamana Bariadi

MIGOGORO ya mara kwa mara kati ya wachimbaji wadogo na wakubwa katika mgodi wa Bulambaka ulioko wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu umeingia katika sura mpya baada ya waandamanaji wadogo kuandamano wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Wachimbaji hao waliandamana hadi ofisi za mkuu wa wilaya huku wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumkataa mwekezaji aliyepewa leseni ya uchimbaji kwenye mgodi huo na Tume ya Madini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari, wachimbaji hao wakiwemo wamiliki wa mashamba, walisema maandamano hayo ni sehemu ya kupaza sauti zao kwa viongozi wakuu kuanzia wilaya hadi taifa. Mmoja wa wachimbaji hao wadogo, Nyakelenge Gidioni alidai mchakato wa kumpata mwekezaji huyo umegubikwa na usiri mkubwa na kuna viashiria vya rushwa katika upatakanaji wake.

“Kwanza hii leseni imetolewa haraka katikati ya kipindi cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli. Tulipouliza kwanini umefanyika kwa usiri na haraka vile wakadai huu ni utawala mpya lazima kila kitu kiende haraka,” alisema Gidioni.

Mchimbaji mwingine, Masunzu Mboje alihoji kama kasi iko hivyo mbona wapo wamiliki wa mashamba katika mgodi huo ambao kwa mwaka mzima wamekuwa wakihangaikia leseni bila mafanikio licha ya kukamilisha taratibu zote.

Alidai mwekezaji huyo baada ya kufika kwenye mgodi huo aliwataka wamiliki wa mashamba kusaini hati ya makubaliano kwa nguvu huku wengine akiwapatia fedha kuwalainisha wasaini.

Aidha, wachimbaji hao walidai mwekezaji huyo amekuwa na vitendo vya unyanyasaji pamoja dhidi ya wawekezaji wadogo. Wachimbaji hao baada ya kufika ofisini kwa mkuu wa wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga aliwaeleza kuwa ofisi yake haitambui leseni hiyo ya mwekezaji na kwamba asingeweza uongelea zaidi mgogoro huo kwani alishatoa maelekezo kwa ofisi ya madini ya mkoa lakini hayajatekelezwa.

“Mimi najua kila kinachoendelea huko na ni kweli leseni hiyo imetoka kinyemela. Ofisi yangu haiitambui ila siwezi kusema zaidi bali niwatake muende kwa mkuu wa mkoa, maana ofisi yangu imeshatoa maelekezo,” alisema Kiswaga.

Akijibu madai dhidi yake, mwekezaji huyo, Hussein Makubi alisema yeye na wenzake wanaounda kikundi cha Buruwadu 4 Mine wamepewa leseni ya kuchimba kwenye mgodi huo na si kweli kwamba leseni ni yake binafsi.

“Na kikundi walichomo hao wenye mashamba mimi ni mwenyekiti. Tupo watu 39 na hizo tuhuma siyo kweli, tulifuata taratibu zote zinazotakiwa na leseni tumepewa kihalali, hakuna vitendo vya rushwa kama wachimbaji wadogo wanavyodai.”

“Tunaomba serikali kuingilia kati kwani shughuli za uchimbaji zimesimama kwa sasa,” alisema. Alipotafutwa Ofisa Madini kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, hakuwa tayari kwani alikua katika kikao cha kamati ya ulinzi na

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Happy Mollel, Simiyu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi