loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zitto apongeza kazi miradi ya kimkakati

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeshauri miradi ya maendeleo ya kimkakati inayotekelezwa na serikali iendelezwe na kasoro zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zifanyiwe kazi.

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa hoja 10 za uchambuzi wa ripoti ya CAG ya 2019/20.

Zitto alisema kasoro alizoanisha CAG katika miradi ya mkakati ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mingine, zirekebishwe na miradi hiyo iendelee kutekelezwa kama ilivyopangwa.

“Tumeona ripoti ya CAG imeainisha kasoro nyingi kwenye miradi mikubwa ya kimkakati, sasa siungi mkono wala sishauri miradi hiyo isitishwe kama baadhi wanavyotaka.”

“Mimi namshauri Rais Samia Suluhu Hassan, kujengwe mfumo mzuri wa uwajibikaji na kuimarisha taasisi imara za serikali zitakazosimamia miradi mikubwa ya serikali ili kuepuka madhara, miradi hii iendelee kwa sababu imeshawekezwa fedha nyingi za Watanzania,” alisema Zitto.

Alisema pamoja na kasoro zilizobainishwa, si sahihi kuacha kuitekeleza ukiwemo ujenzi mradi wa kuzalisha umeme katika bonde la Mto Rufiji. Kuhusu kampuni ya ndege (ATCL) alisema ACT-Wazalendo inashauri serikali kulisuka upya shirika hilo kwa sababu inaokenaka kuna tatizo la kimuundo na umiliki.

Zitto alisema, pamoja na hasara zilizobainishwa na CAG, kuna matumaini makubwa katika shirika la ATCL, hivyo unahitajika uammuzi sahihi. “Katika hili tunapendekeza muundo wa umiliki wa ATCL ubadilishwe kwa kuhusisha mashirika ya uhifadhi na utalii kama wamiliki.

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wamilikishwe asilimia 60 ya kampuni,” alisema. Alisema baada ya kumilikishwa, Tanapa na NCAA waondolewe katika orodha ya mashirika yanayopeleka hazina asilimia 15 ya makusanyo gha

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi