loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali Uganda yapendekeza ada leseni za magari

WIZARA ya Fedha imependekeza ada ya leseni ya kila mwaka ya Sh 200,000 kwa wamiliki wote wa magari kama sehemu ya vyanzo vya mapato katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Waziri wa Fedha, David Bahati amesema hatua hiyo pia inakusudiwa kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa kuondoa magari haramu na kukusanya fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara nchini.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, wamiliki wa gari watatakiwa kulipa Sh 200,000, wakati wamiliki wa pikipiki watalipa Sh 50,000 kila mwaka.

Waziri huyo alisema hayo  mbele ya Kamati ya Fedha ya Bunge  na kwamba wanapendekeza ada hiyo ianze kutozwa Julai 1, 2021 baada ya kuingizwa katika Muswada wa  Marekebisho ya Sheria mbalimbali.

Hatua hiyo ina maana ili mtu aweze kuingiza gari barabarani, anatakiwa kuwa na leseni ya barabara  badala ya leseni ya udereva na atakayeshindwa  kulipia leseni ya barabara anaweza kufungwa jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh milioni 2 au vyote kwa pamoja.

Bahati aliiambia kamati hiyo  kuwa ikiwa leseni hiyo itapitishwa, nchi itakuwa na magari yanayostahili barabara na wakati huo huo serikali itapata fedha za kuboresha  barabara.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi