loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wataka fidia kuipa serikali soko

WAFANYABIASHARA wa soko la Nakasero wameitaka serikali iwalipe fidia ya Sh bilioni 300 kama inataka kulichukua kuliendesha.

Wamesema hayo kutokana na azimio la Baraza la Mawaziri kutaka masoko yote ya umma jijini Kampala yamilikiwe na serikali ili kupunguza changamoto katika  usimamizi.

Wafanyabiashara hao kupitia wakili wao, Paul Kenneth Kakande wamesema wana hati ya kumiliki eneo hilo kwa miaka 49 na kwamba serikali kuchukua eneo hilo kutawasababishia  hasara kubwa.

Wafanyabiashara  walikodisha eneo hilo kutoka Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) kwa Sh bilioni 2 wanatakiwa kulipa kodi ya ardhi ya Sh milioni 90 kila mwaka.

Kakande alisema serikali haikuangalia vizuri masuala ya  kisheria yanayozunguka soko la Nakasero na badala yake imeagiza KCCA kuchukua kituo hicho mara moja.

Alisema ingawa sheria inaruhusu serikali kuchukua ardhi, lakini inapaswa kufanywa hivyo kisheria kwa kulipa fidia wenyeji ambao wana haki na ardhi husika.

 "Wafanyabiashara wana mkataba ambao bado unaendelea na wana matarajio ya kufanya biashara kwenye ardhi hiyo na ndiyo sababu walichanga fdha kukodisha ardhi. Kwa hivyo kama unalihitaji eneo lazima ulipe fidia kulingana na matarajio yao  ya kile wangeweza kupata katika miaka 49,”alisema.

Alisema soko la Nakasero haliko tu katika eneo muhimu la kipaumbele kufanya biashara, lakini lina  wafanyabiashara zaidi ya 5,000 wanaofanya biashara kwa lengo la kupata faida.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi