loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Biashara ndogo 750,000 kutafutiwa soko kimataifa

MAMLAKA ya Uwekezaji Uganda (UIA) imeorodhesha biashara ndogo na za kati 750,000 kwa nia ya kuziunganisha na masoko ya kimataifa.

Biashara hizo ambazo zilianza kuorodheshwa Novemba mwaka jana, zitakutanishwa na kampuni za kimataifa zinazoingiza bidhaa nchini.

Aidha, mamlaka hiyo itawasaidia wajasirimali hao kuboresha viwango vya bidhaa zao na vile vile kukuza biashara hizo katika huduma na kufikia kuwili ziwe ziweze kukubalika kimataifa.

Naibu Mkurugenzi wa UIA,  Paul Kyalimpa alisema juzi kuwa, kwa kuorodhesha biashara hizo, mamlaka hiyo inataka kuwawezesha wajasirimali wadogo na wakati wafikie ubora na kupata vyeti vya bidhaa zao kuwa vya viwango vya kimataifa.

"Tunawahamasisha kupitia Taasisi ya Utafiti wa Viwanda ya Uganda kufikia viwango fulani ambavyo vinahitajika na kampuni za kimataifa," alisema.

Biashara ndogo na za kati nchini zimekuwa zikikumbwa na changamoto kadhaa, kati ya hizo ni ukosefu wa soko, upatikanaji mdogo wa mitaji na viwango duni vya bidhaa zinazozalishwa.

Kyalimpa alisema biashara hizo zinatakiwa kukuzwa ili kuwa biashara kubwa kwasababu  zinachangia asilimia 80 ya uchumi wa Uganda.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi