loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanajeshi wa UN nchini kupunguzwa asilimia 7

UJUMBE  wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umesema mwaka huu una mpango wa kupunguza idadi ya wanajeshi wake kwa asilimia saba kutokana na kupungua kwa vurugu.

Mkuu wa UNMISS Sudan Kusini, David Shearer amwsema hatua hiyo  ni matokeo ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka  katika kambi ambazo raia walikuwa wameomba ulinzi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka sita.

"Mwaka ujao kutakuwa na upunguzaji wa walinda amani wa jeshi na polisi kwa karibu asilimia saba," Shearer aliwaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wake wa mwisho baada  ya  kufanya kazi nchini kwa miaka minne.

Alisema uamuzi huo pia umetokana na kupungua kwa vurugu baada ya kutiwa saini  makubaliano ya amani mwaka  2018.

UNMISS hivi sasa ina wanajeshi 14,500 na walinda amani na polisi 2,000 nchini.

Shearer amewahimiza viongozi kuongeza  kasi ya utekelezaji wa katiba mpya, uundaji wa jeshi la kitaifa na mageuzi ya kiuchumi.

Takribani watu  400,000 wanakadiriwa kufa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka mwaka  2013 ikiwa ni miaka miwili baada ya Sudan Kusini kupata  uhuru kutoka kwa Sudan.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: JUBA, Sudan Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi