loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sudan Kusini, Sudan kushirikiana mafuta

SUDAN na Sudan Kusini zimekubaliana kushirikiana katika sekta ya mafuta.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa  mkutano wa kati ya Waziri wa Nishati na Mafuta wa Sudan, Gadain Ali Ebaid na mwenzake wa Sudan Kusini, Puot Kang.

Wakati wa makubaliano hayo, Ebaid alisema sekta ya mafuta ni kipaumbele kwa watu wa nchi hizo mbili na kutaka kuwekwa mikakati zaidi katika ushirikiano wa nchi hizo katika sekta hiyo.

Septemba mwaka jana, Sudan na Sudan Kusini zilitia saini makubaliano ya rasimu ya kukuza ushirikiano katika sekta ya mafuta.

Aidha, nchi hizo zimekubaliana kuimarisha uhusiano kwa kuwezesha harakati za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi.

Uamuzi huo ulifikiwa kati ya Waziri wa Uwekezaji wa Sudan, Dk Al-Hadi Mohamed Ibrahim na mwenzake wa Sudan Kusini, Dhieu Mathok.

Ibrahim alisema ushirikiano wa kati ya nchi hizo mbili ni miongoni mwa vipaumbele vya serikali.

Kwa upande wake, Mathok alitaka kudumishwa ushirikiano wa karibu na uratibu kati ya wizara hizo mbili na kufunguliwa tena kwa mipaka  kati ya nchi hizo mbili.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: JUBA, Sudan Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi