loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

WFP kupunguza msaada wa chakula kwa wakimbizi

SHIRIKA la Chakula Duniani (WFP) limesema litapunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi takribani  700,000 wa ndani na nje nchini Sudan Kusini.

Mwakilishi wa WFP nchini,  Matthew Hollingworth alisema juzi kuwa, kuanzia mwezi huu wakimbizi wataanza kupokea asilimia 50 ya mgawo kamili wa chakula badala ya  asilimia 70.

Shirika hilo limesema rasilimali zake Sudan Kusini zimepunguzwa wakati ambapo viwango vya ukosefu wa chakula viko juu zaidi katika kipindi cha muongo mmoja na wafadhili wanakabiliwa na athari za kiuchumi za covid-19.

"Lazima tujaribu kuokoa maisha ya wanaokabiliwa na njaa ambao hawatapata msaada wa kutosha. WFP haina rasilimali za kutosha kutoa mgawo kamili kwa wote ambao wanategemea msaada wetu kuishi nchini Sudan Kusini,” alisema Hollingworth.

WFP imesema inahitaji dola za Marekani milioni 125 kwa ajili ya shughuli zake za msaada wa chakula kwa miezi sita ijayo ili kutoa chakula cha kutosha kwa idadi ya wakimbizi waliopo.

Walioathiriwa inasemekana ni pamoja na wakimbizi wa ndani 440,000 waliopo Bentiu, Bor, Juba, Malakal, Mingkaman na Wau na karibu wakimbizi 260,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia na Sudan, ambao wanategemea msaada wa WFP kukidhi mahitaji yao chakula.

Mashirika ya misaada yamesema hali imezidi kuwa mbaya kote nchini, kwani watu takribani  milioni 7 au asilimia 60 ya idadi ya watu wanahangaika kupata chakula cha kutosha kila siku.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: JUBA, Sudani Kusini

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi