loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waathirika mauaji ya kimbari wakumbukwa

WAATHIRIKA zaidi ya 97,000 wa mauaji ya kimbari katika mkoa wa Nyanza wamekumbukwa kwa sala na maombi kwenye makaburi ya Kicukiro katika mji wa Nyanza.

Wananchi wa Rwanda wapo katika siku 100 za maadhimisho ya miaka 27 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu wa kabila la Watusi waliuawa.

Miongoni mwa mauaji mabaya kabisa katika historia ya Rwanda ni mauaji ya watu zaidi ya 2,500 waliouawa kwa pamoja baada ya kutelekezwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Watu hao waliokuwa wamejificha katika eneo moja liitwalo ETO – Kicukiro kwa sasa likijulikana kwa jina la IPRC – Kigali wakiwa wanalindwa na askari wa Ubelgiji chini ya Umoja wa Mataifa (UNAMIR) na kuwaacha bila ulinzi ambapo walivamiwa na wanamgambo wa Interahamwe.

Meya wa Jiji la Kigali, Pudence Rubingisa amewaasa vijana kujituma kutafuta historia ya mauaji hayo pamoja na  kutembelea makumbusho mbalimbali ili kujipa ufahamu wa nini kilifanyika mwaka 1994  na kujua maana ya mauaji ya kimbari.

“Kwa kutembelea makumbusho mbalimbali, wale wote ambao walikuwa wakikataa na kupinga uwapo wa mauaji ya kimbari watapata uelewa na kuondoa fikra potofu vichwani mwao,”  alisema Rubingisa.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: NYANZA, Rwanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi