loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kamati za Maadili Taasisi za Umma zafundwa

MAFUNZO  ya kudhbiti uadilifu kwa Kamati za Maadili kwa Taasisi za umma yameazinduliwa leo Makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki yaliyopo jijini Arusha.

Washiriki wa mafunzo hayo wametakiwa kuhakikisha wanasimamia na kukuza maadili ya watumushi wa umma katika taasisi zao.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Dk. Remigius Kawala akifungua mafunzo hayo ambapo alisema uwepo wa kamati hizo  za maadili katika taasisi za umma  ni lengo la serikali kujali na kusimamia maadili mema kwa wafanyakazi wake.

“Hizi kamati zinalengo la kusimamia madili mahala pa kazi na kuondoa ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya watumishi wa umma unaosababisha uwepo wa masuala mbali mbali yakiwemo vitendo vya rushwa, ulevi, uonevu, wizi na matendo mengine yasiyo na staha kwa jamii, hivyo naamini haya mtayajadili kwa kina katika kuleta ufumbuzi wake  huko kwenye kamati zenu” alisema Dk. Kawala.

Baadhi ya masuala yatakayojadiliwa kwenye mafunzo haya ni pamoja na kanuni za maadili ya utumishi wa umma na namna ya kushughulikia malalamiko mbali mbali ya kimaadili,mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa, dhana ya rushwa mahala pa kazi na dhana ya mgongano wa maslahi.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi