loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfanyabiashara kortini akidaiwa kughushi akope milioni 350/-

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imempandisha kizimbani mfanyabiashara John Kyenkungu akikabiliwa na mashitaka ya kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa Sh milioni 350 kutoka benki ya Equity.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Adolph Lema, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mbando.

Wakili Lema alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka mawili ya kughushi. Katika shitaka la kwanza inadaiwa katika tarehe zisizofahamika mwaka 2014 ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam kwa nia ya kufanya udanganyifu, Kyenkungu alighushi hati ya mkopo ya mwaka 2014.

Ilidaiwa mahakamani kuwa, mshitakiwa huyo alisaini kuwa Said Nasoro alikubali kutumia hati ya nyumba yenye namba 25480 ya Kiwanja Namba 516 Kitalu B iliyopo Mikocheni, Kinondoni mkoani Dar es Salaam kama dhamana ya mkopo wa Sh milioni 350 kutoka benki ya Equity huku akijua si kweli.

Wakili Lema alidai kuwa, Agosti 23, 2014 mshitakiwa huyo alighushi barua iliyoonesha kuandikwa katika tarehe hiyo kwa kusaini kuwa Said Nasoro alikubali kutoa hati ya nyumba kama dhamana ya mkopo huo.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kupelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika watakaosaini bondi ya Sh milioni 100 kila mmoja na yeye mshitakiwa kulipa benki Sh milioni 75.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Aprili 21 mwaka huu itakapotajwa.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi