loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mpango wa kitaifa kuvuna maji ya mvua waandaliwa

WIZARA ya Maji inaandaa mpango wa kitaifa  utakaohusisha wananchi katika kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya matumizi mbalimbali na kuepuka majanga.

Wizara hiyo imesema, kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mpango huo utahisisha shule kujenga gata za maji na matanki pamoja na kuhamasisisha wananchi wanapojenga nyumba zao waweke miundombinu rafiki ya kukusanya maji ya mvua.

Naibu Waziri wa Maji, Maryprica Mahundi alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Zainabu Katimba (CCM) aliyetaka kujua serikali imejidhatiti vipi kuhamasisha uvunaji wa maji ya mvua kwa matumizi ya wananchi.

Alisema Tanzania ipo kwenye ukanda wenye mvua za kutosha, hivyo ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ni muhimu ili kuwa maji ya uhakika kwa kipindi chote cha mwaka bila kujali hali ya hewa.

Aidha, alisema miundombinu hiyo ni muhimu kwani itawezesha kudhibiti mafuriko na hivyo kuokoa miundombinu mingine pamoja na mali na maisha ya wananchi.

Mahundi alisema katika kuhakikisha uvunaji wa maji unawezekana, serikali itaendelea na ujenzi na ukarabati wa mabwawa kwa katika kila wilaya hususan katika zilizo kame.

Alisema katika mwaka wa fedha 2020/21, Wizara ya Maji imekamilisha ukarabati wa bwawa la Mwadila wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu na usanifu kwa ajili ya kukarabati mabwawa matatu  ya Itobo liliopo wilaya ya Nzega.

Alisema pia bwawa la Engukument wilayani Monduli na Horohoro wilaya ya Mkinga yatafanyiwa ukarabati pamoja na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa mawili ya Muko na Chiwanda yaliyopo wilaya ya Momba.

Aidha, alisema usanifu wa Malambo ya kunyweshwea mifugo sita  umekamilika katika mwambao wa barabara kuu ya Dodoma-Babati ikihusiha wilaya za Bahi (malambo mawili)  na Chemba (malambo manne).

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi