loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Anglogold Ashanti, BG Umoja zaingia ubia kuchimba madini

KAMPUNI ya Anglogold Ashanti ya Afrika Kusini imeingia ubia na Kampuni ya BG Umoja ya nchini kwa ajili ya kuchimba madini katika miradi ya Nyankanga na Geita Hill.

Anglogold ambayo ni kampuni mama ya Geita Gold Mine (GGML) imeipatia BG Umoja mkataba wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 186 kwa miaka miwili.

Kazi za BG Umoja zitafanywa kampuni ya Africa Underground Mining Services (AUMS) ya Tanzania kwa asilimia 80, kampuni tanzu ya kundi la Perenti Australia na kampuni ya huduma za uchorongaji wa ndani na usambazaji madini ya Geofields Tanzania Limited itakayopewa kazi kwa asilimia 80.

Akizungumzia ubia huo, Ofisa Uendeshaji Mkuu wa AngloGold Ashanti –Afrika, Sicelo Ntuli alisema : “Tunafanya kazi na wakandarasi wa uchimbaji wenye uzoefu watakaotusaidia kuwezesha uhamisho wa muda mrefu wa ujuzi endelevu, na kuendelea kujenga mipango endelevu ya manunuzi ya ndani.”

“AngloGold Ashanti inajenga mipango endelevu ya manunuzi ya ndani itakayochochea maendeleo ya uchumi na jamii katika miradi, inayoshuhudiwa na mchango mkubwa kutoka Geita Gold Mining Limited ambao umechangia mapato makubwa ya watu wa Tanzania,” alisema.

Alisema matumizi ya mwaka ya AngloGold Ashanti kwa watoa huduma Watanzania wazawa yameongezeka hadi Dola za Marekani milioni 162 kuanzia mwaka 2016.

“Timu ya kusimamia manunuzi ya ndani imejiwekea malengo makubwa ya asilimia 60 hadi 70 ya matumizi yote kufanywa na kampuni za Kitanzania ifikapo 2025.”

“Kampuni ya AngloGold Ashanti - Geita Gold Mining Limited imetoa pia mkataba wa miaka miwili wa usafirishaji mafuta wenye thamani ya Dola milioni 10.8 kwa mwaka kwa kampuni mbili za Kitanzania,” alisema Ntuli.

Mojawapo ya kampuni kati ya mbili zitakazonufaika katika mkataba huo ina asili ya Geita na inathibitisha ahadi ya GGML kuwezesha uchumi wa jamii wenyeji,” alisema.

Alisema kampuni ya Geita itakayonufaika katika mpango huo imepatikana baada ya jitihada za GGML kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kutoa mafunzo wezeshi kwa watoa huduma wa Geita ili kuongeza wigo wa kushindana katika manunuzi na utoaji huduma unaofanywa na mgodi.

Ntuli alisema: “Katika kufikia viwango vya kimataifa, malori ya kubeba mafuta hayo yamepewa mwongozo wa kuzingatia utoaji moshi kwa mujibu wa viwango vya EURO IV, matangi yanapaswa kutengenezwa kwa kutumia aluminium ili kupunguza uzito na kila gari litapaswa kutumika katika kipindi kisichozidi miaka sita.”

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi