loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ yatangaza bei mpya ya karafuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza bei mpya ya karafuu kwa msimu wa mavuno wa mwaka huu huku ikishuka kutoka Sh 14,000 hadi Sh 10, 350.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban akizungumza na waandishi wa habari alisema bei ya zao hilo itakuwa ikiendana na bei halisi kwenye soko la dunia.

‘’Bei ya karafuu kwa msimu wa mavuno wa mwaka huu itakuwa kilo moja Sh 10,350 badala ya bei ya zamani ya kilo moja Sh 14,000...serikali itakuwa ikinunua karafuu kutoka kwa wakulima kwa bei ya soko ilivyo,’alisema Shaaban.

Alisema bei ya karafuu itakuwa ikipanda na kushuka kulingana na hali ya soko la dunia. Shaaban alisema katika utaratibu wa mabadiliko ya bei ya zao hilo mkulima atakuwa akipata asilimia 80 ya bei ya sokoni ya kuuza karafuu yake.

Alisema serikali imelazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kuweka bei ya karafuu ya kilo moja Sh 10, 350 na kwamba, ugonjwa wa Covid- 19 kwa kiasi kikubwa umevuruga mwenendo wa bei na hali ya soko na uchumi kwa ujumla.

Aliwataka wakulima wasikate tama, waoneze juhudi ya uzalishaji wa zao la karafuu kwa kuwa bei inaweza kupanda kulingana na hali ya soko la dunia lilivyo.

Shaaban alisema serikali itaendelea kutoa mikopo nafuu kwa wakulima katika kuendeleza kilimo hicho pamoja na kujenga miundombinu yaa kilimo cha karafuu na mashamba ya wakulima.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi