loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mitungi 400 ya gesi yabambwa yakiwa na ujazo hafifu

WAKALA ya Vipimo (WMA) Mkoa wa Kilimanjaro imekamata zaidi ya mitungi 400 ya gesi za matumizi ya majumbani ikiwa na ujazo pungufu. Kaimu Meneja wa WMA wa mkoa huo, Dennis Misango alisema jana kuwa walikamata mitungi hiyo baada ya kufanya operesheni ya ukaguzi.

Aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake mjini Moshi kuwa walifanya ukaguzi katika vituo vya kujazia gezi vya kampuni nne na kubaini kampuni moja ilikuwa inajaza gesi pungufu katika mitungi ya kilo sita.

“Tumefanya ukaguzi na tulibaini kuwa mitungi mingi ya kilo sita ilikuwa imejazwa pungufu na kuikamata yote 400 ambapo tuliitaka kampuni husika kuirejesha kiwandani na kuijaza tena kwa lengo la kumlinda mlaji”alisema Misango.

Alisema, baada ya kuikamata mitungi hiyo waliipiga faini kampuni hiyo ya zaidi ya shilingi milioni nane ili iwe fundisho kwa kampuni nyingine.

Misango alisema, ukaguzi huo ulibaini kuwa ni mitungi ya kilo sita pekee iliyokuwa imejazwa pungufu na kwamba yenye ujazo tofauti ilikuwa imejazwa kwa usahihi

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Upendo Mosha, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi