loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Soko la Bidhaa marufuku udalali mazao ya wakulima

SERIKALI imepiga marufuku Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kufanya kazi za udalali wa mazao ya wakulima badala yake lijikite katika kutafuta masoko ya mazao nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alitangaza uamuzi huo jana bungeni Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za malalamiko zilizoibuliwa na wabunge wakati wakichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa Jumanne Aprili 13, mwaka huu.

Bashe alisema Wizara ya Kilimo imelifanyia kazi suala la TMX ili kuhakikisha inaacha kujishughulisha na shughuli za minada, kwani walifanya majaribio mwaka jana walipata matokeo na sasa na hivyo ushirika utafanya shughuli hizo.

“TMX inatakiwa kuachana na shughuli za minada na kurudi katika kazi zake za msingi za kutafuta masoko ya mazao nje ya nchi,” alisema Naibu Waziri.

Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga (CCM) alisema serikali inatakiwa kuangalia namna itakavyoweka mikakati ya kusaidia wakulima badala ya kuruhusu TMX kuwapora wakulima mazao.

“Lakini TMX pamoja na kuwa ni taasisi ya serikali chini ya wizara ya fedha na mipango, ambayo wajibu wake wa msingi ni kutafuta masoko ya nje, imeacha majukumu yake hayo,” alisema Silanga.

Alisema mwaka 2018, TMX badala ya kutafuta masoko ya pamba nje ya nchi, iliingilia kati na kutafuta asilimia moja kwenye ushirika wa wakulima wa zao hilo.

Mbunge wa Magu, Bonaventura Kiswaga (CCM) wakati akimpata taarifa mbunge huyo wa Itilima, alisema TMX imejiondoa katika kutafuta masoko nje ya nchi, badala yake imejigeuza kuwa dalali kwenye minada ya mazao.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) alipongeza serikali kuiondoa TMX katika shughuli za kuwa dalali katika mazao ya wakulima badala yake irudi kufanya kazi zake za kutafuta masoko ya mazao nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Hassan Selemani Mtenga (CCM) alimpongeza Bashe kwa kuwa msikivu na kupiga marufuku TMX kujishughulisha na udalali.

Mtenga alisema mkoani Mtwara ambako zao la korosho linalimwa, TMX ilikuwa dalali kwa wakulima na kuanzisha mfumo wa kuuza na kununua zao hilo kwa njia ya mtandao kitendo ambacho kimewanyika ajira.

Alisema wanunuzi wa korosho wapo Vietnam na India hivyo kutokana na mtindo wa TMX wa kuuza kupitia mtandao, wafanyabiashara wengi waliopo Mtwara wamepoteza ajira kwani ununuzi unafanyika kwa njia ya mtandao.

TMX ni soko la bidhaa Tanzania ambalo wajibu wake wa msingi ni wauzaji na wanunuzi wanakutana na kubadilishana bidhaa na fedha katika mtindo wenye mpangilio na utaratibu maalumu na kwa kanuni mahususi na zenye uwazi zilizoelezwa vizuri

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi