loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchakato tathmini ya athari kwa mazingira kuanza

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo kesho Jumamosi anakutana na wadau wa mazingira kujadili masuala ya mchakato wa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira (TAM/EIA).
Wadau watakaoshiriki mkutano huo ni pamoja na wawekezaji, washauri elekezi wa mazingira pamoja na Taasisi na watu binafsi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk Samuel Gwamaka alibainisha kuwa umelenga kuainisha na kuzitatua changamoto zilizopo katika ufanyaji wa tathmini ya athari ya mazingira na kupata maoni yatakayoboresha ufanyikaji wa tathmini.
Alisema kwa kuwa kabla ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wowote mkubwa wa uwekezaji ni lazima kuwepo na cheti cha tathmini ya athari za mazingira ambacho hutolewa na waziri mwenye dhamana.
Alisema kumekuwa na changamoto kadhaa katika utekelezwaji wa takwa hilo hivyo kuchelewesha baadhi ya miradi ya uwekezaji hasa ambao unahitaji kwanza cheti hicho.
Alisema kutokana na changamoto hizo, kumeibuka na malalamiko mengi kutoka kwa wadau ambapo Waziri Jafo ameamua kukutana nao kusikiliza maoni yao kwa lengo la kupata mustakabali wa suala hilo.
Alisema mkutano huo utatoa majibu na kupokea mapendekezo ili tathmini zifanyike kwa ufanisi na kwa wakati.
“NEMC inawakaribisha katika mkutano huo wadau wote ili kutoa maoni yao na watakutana na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa waziri Jafo na wataalamu wake pamoja na kupanga kwa pamoja njia za kurahisisha upatikanaji wa cheti cha tathmini ya mazingira,” alisema Dk Gwamaka.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi