loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ulega: Tunafanya maboresho sera, sheria ya uvuvi

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema inaendelea kufanya maboresho makubwa ya sera na sheria ya uvuvi nchini, ili kuendana na mahitaji halisi ya sasa ya kisekta, ikiwemo kutatua kero mbalimbali za wadau wa sekta hiyo hususan wavuvi wadogo na wakuzaji viumbe maji.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, ameeleza hayo leo bungeni Dodoma wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri, lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira, lililolenga kujua utayari wa wizara hiyo kupitia upya sera na sheria ya uvuvi nchini kukidhi mahitaji ya wavuvi wadogo.

Amesema katika kutekeleza hilo wizara imekuwa ikifanya mapitio ya sera, Sheria na kanuni za uvuvi ili ziweze kuendana na mahitaji halisi ya wakati husika, na imekuwa ikifanya hivyo mara kwa mara.

“Kwa mfano wizara ilifanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Uvuvi na mikakati yake ya mwaka 1997 na kutunga  Sera ya Taifa ya Uvuvi ya mwaka 2015, ambayo imezingatia mahitaji ya wadau wa sekta ya uvuvi na uendelevu wa rasilimali za uvuvi,”  amesema Ulega.

 Ameongeza kuwa mapitio na marekebisho ya sheria ya uvuvi yamesaidia kuimarisha shughuli za utafiti, ulinzi na usimamizi shirikishi wa rasilimali za uvuvi, nchini.

 

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Isdori Kitunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi