loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ YATOA NENO MASHEHE WA UAMSHO WANAOSHIKILIWA

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wananchi kuwa watulivu na subra huku suala la kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa mashehe saba wa kundi la Kiislamu la Uamsho likifanyiwa kazi na kufuatiliwa kwa karibu.

Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman (pichani) alisema hayo wakati akizungumza na Waislamu katika sala ya Ijumaa,juzi katika msikiti wa 

Mahufira hapo Mchangani mjini Unguja. Othman alisema Serikali inafuatilia kwa karibu suala hilo na kwamba lipo katika mkondo wa taratibu za kisheria na si vyema kuliingilia kati . Alisema busara ni muhimu zaidi kutumika katika pande mbili za mazungumzo.Alifafanua kwamba si kweli kwamba suala la kushikiliwa kwa viongozi hao wa uamsho limeachwa na hakuna kiongozi anayelishughulikia kwa upande wa Zanzibar.

‘’Napenda kuwajulisha wananchi ikiwemo waumini wa dini ya Kiislamu kwamba suala la kukamatwa kwa viongozi hao lipo katika mkondo wa kisheria na si vyema kuliingilia kati....Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia viongozi wake wanalifuatilia kwa karibu sana,’’alisema.

Viongozi wa kundi la Kiislamu la Uamsho wakiongozwa na Shehe Farid Hadi Suleiman walikamatwa na Jeshi la Polisi Zanzibar kati ya Agosti 17 na 18 mwaka 2012 kwa  kusababisha vurugu na kufanya maandamano kinyume na sheria.

Viongozi hao walifikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe Oktoba 21 mwaka 2012 kujibu tuhuma zinazowakabili za vurugu na maandamano yaliyosababisha kutishia maisha ya wananchi na kuyumba kwa sekta ya watalii.

Awali, Othman aliwataka wananchi kuendelea kuombea dua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarika kwa amani na utulivu wa wananchi wake kutokana na mabadiliko makubwa yaliyojitokeza nchini.

Aliwataka Waislamu kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza Tanzania iendelee kuwa na utulivu kwa wananchi wake kuishi kwa amani na kupiga hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi.

Aidha aliwataka Wazanzibari kuendelea kudumisha maridhiano ya kisiasa ambayo yamesaidia na kufungua milango ya maelewano na nchi kuwa na utulivu wa kudumu unaotowa nafasi wananchi kufanya shughuli za maendeleo na uchumi.

‘’Tunapaswa pia kuyaombea dua maridhiano yetu ambayo yamefungua milango ya heri na mafanikio na ndiyo maana hivi sasa tunaishi vizuri kwa maelewano’’alisema

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi