loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mume aua mke, mtoto naye ajijeruhi

MKAZI wa Kijiji cha Buhanga, Kata ya Buganguzi wilayani Muleba, Joackim Rwegasira (45) anatuhumiwa kumuua mkewe na mtoto wa mwaka mmoja naye kujijeruhi tumboni na shingoni kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Maketi Msangi alimtaja aliyeuawa ni Rosemary Joackim mwenye umri wa miaka 35 na mtoto wake, Joines Joackim.

Kwa mujibu wa kamanda, mtuhumiwa huyo ambaye alitaka pia kujiua, anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika juzi saa 9:00 alasiri nyumbani kwake.

Msangi alisema, chanzo cha mauwaji hayo ni wivu wa mapenzi kutokana na Joackim kumtuhumu mkewe kuwa alikuwa na mahusiano na jirani yake na kudhaniwa kuwa mtoto aliye naye si wake.

“Akiwa mtaani watu walimwambia kuwa mtoto huyo sio wa kwake ni wa jirani yake ambapo kabla ya mauaji hayo alipeleka ma-

lalamiko ngazi za kijiji kwa maana ya mwenyekiti wa kijiji lakini kabla maamuzi ya mwenyekiti kuwapatanisha yeye na mkewe, akaamua kufanya mauaji,”alisema Msangi

Alisema, baada ya mauaji, mwanaume huyo alijijeruhi tumboni na shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali kwa lengo la kutaka kujiua.

Alisema kuwa, uongozi wa kijiji na Polisi wilayani Muleba walikuta miili imelazwa chumba kimoja na na yeye kukutwa sebuleni akiwa na hali mbaya.

Alisema mtuhumiwa anaendelea na matibabu katika hospitali teule ya Wilaya Rubya kwani hali yake ni mbaya na kwamba akipona atafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Diana Deus, Muleba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi