loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Samia ateua katibu wake, wasaidizi

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi mbalimbali ikiwamo wa Katibu wake kwa kumteua Juma Mkomi kushika nafasi hiyo.

Sambamba na uteuzi wa wasaidizi katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) sita kwenye maeneo mbalimbali, vile vile amemteua Said Juma kuwa Mnikulu.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya habari juzi, imetaja wasaidizi hao ni Balozi Dk Mussa Lulandala anayekuwa Msaidizi wa Rais, Nyaraka na Ukalimani.

Wasaidizi wengine wa rais na maeneo yao ya kazi kwenye mabano ni Balozi Ali Sakila (Hotuba), Maulidah Hassan (Diplomasia) na Feilister Mdemu anayekuwa Msaidizi wa Rais, Maendeleo ya Jamii.

Rais Samia pia amemteua Nehemia Mandia kuwa Msaidizi wa Rais, Sheria, Dk Blandina Kilama (Uchumi) na Dk Salim Othman kuwa Msaidizi wa Rais, Siasa.

Taarifa hiyo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilisema kuwa uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi