loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Katibu mambo ya nje atembelea miradi Bonde la Ziwa Victoria

KATIBU Mkuu , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amehitimisha ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoratibiwa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria.

Balozi Brigedia Jenerali Ibuge alikuwa katika ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lakini kwa kushirikiana na sekta nyingine hususani maji pamoja na uchukuzi.

“Tumekuwa tukitembelea kuona utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ambayo inaihusu nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Uganda lakini pia Sudani ya Kusini,” alisema.

Alisema lengo hasa la ziara hiyo ni kutambua utekelezaji huo unavyoendelea wa miradi ambayo inagusa wananchi zaidi ya milioni 40 katika nchi tano za Afrika Mashariki zinazohusisha Bonde la Ziwa Victoria, lakini pia kuangalia changamoto zilizopo kwa lengo la kuwezesha utatuzi unaofaa.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi