loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KAGERE AMHOFIA DUBE

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, anamhofia mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube katika mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Mabao mawili aliyofunga Kagere kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yalimpandisha kileleni mwa mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 11, huku Dube akibaki nafasi ya pili na mabao yake 10.

Kinara huyo wa mabao kwa misimu miwili mfululizo, amezungumza na gazeti hili na kueleza kuwa kinachosababisha amhofie Dube ni muda mchache anaopata kwenye timu yake ya Simba, tofauti ilivyokuwa misimu iliyopita ambapo alikuwa akicheza dakika zote 90.

“Dube ndiye ninayemhofia kwenye mbio za ufungaji bora msimu huu, sababu amekuwa akifanya vizuri kila anapopata nafasi ya kucheza kwenye timu yake na bahati mbaya kwangu msimu huu sipati muda mrefu wa kucheza,” alisema Kagere.

Mshambuliaji huyo alisema pamoja na changamoto hizo amejipanga kukabiliana nazo na kuzishinda kwa kufunga mabao kila atakapopewa nafasi ya kucheza hata kama ni dakika 10.

Katika mchezo dhidi ya Mtibwa ambao Simba ilishinda 5-0 Kagere alicheza dakika 90.

Kagere alieleza kuwa Simba imekuwa na viungo bora wenye uwezo wa kutengeneza nafasi, hivyo hata kama akipewa nafasi dakika chache anaamini anaweza kufunga.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi