loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi awahakikishia Wasabato ushirikiano

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameuhakikishia uongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Tanzania kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kushirikiana nao kwani inatambua mchango wao katika kusaidia huduma za jamii hapa nchini.

Dk Mwinyi aliyasema hayo juzi Ikulu mjini Unguja alipokutana na uongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania uliofika kwa ajili ya kujitambulishakwake na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Nane, ukiongozwa na Askofu Mark Malekana.

Dk Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake kwa kanisa hilo kutokana na kuthamini mchango wake katika kutoa huduma za jamii hapa nchini.

Alisema kanisa hilo limeweza kuwajenga kiimani waumini wake na kushirikiana na serikali kuimarisha sekta za elimu na afya kwa Unguja na Pemba.

Alifahamisha kwamba serikali itakuwa tayari kuhakikisha miradi inayoanzishwa na kanisa hilo ikiwemo ya elimu na afya inafikia malengo yaliyokusudiwa katika kutoa huduma kwa jamii.

Alilipongeza kanisa hilo kwa kusaidia kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha huduma za jamii zikiwamo za elimu kwa kusaidia kuimarisha wa sekta hiyo katika Shule ya Ali Khamis Camp iliyopo Pemba kwa kusaidia walimu wa sayansi pamoja na vitabu.

Katika mazungumzo hayo, Askofu Mark Malekana ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania akiwa na ujumbe wake wa maaskofu kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, alimpongeza Rais Mwinyi kwa kuchaguliwa kwa ushindi mkubwa na wananchi wa Zanzibar.

Aidha, Askofu Malekana alimpongeza Dk Mwinyi kwa kasi kubwa ya kuiletea maendeleo Zanzibar aliyoanza nayo ikiwa ni pamoja na maono yake ya uchumi wa buluu huku akiahidi kwamba kanisa lake litaendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufikia malengo yake iliyojiwekea.

Askofu Malekana alimueleza Dk Mwinyi kwamba Kanisa la Waadventista wa Sabato limekuwa likipata ushirikiano mzuri kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusisitiza haja ya kuimarishwa zaidi.

Akitoa historia ya Kanisa hilo, Askofu Malekana alisema kwa Zanzibar kanisa hilo lilianza mwaka 1986 na kwamba, kuanzishwa kwake kuliambatana na utoaji wa huduma za kiroho na kijamii.

Alisema katika huduma za kijamii, kanisa hilo lilianzisha huduma za utabibu kwa kuwa na vituo viwili vya afya Unguja na Pemba na kuanzisha shule ya awali na msingi huko Tomondo.

Kwa sasa Kanisa hilo lipo katika hatua za kuanzisha shule ya sekondari.

Kwa upande wa Pemba, alisema kanisa hilo lilitoa vitabu katika Shule ya Ali Khamis Camp vyenye thamani ya Sh milioni nne pamoja na kutuma walimu wawili wa masomo ya sayansi waliokuwa wakihudumiwa na kanisa kwa miaka mitano mfululizo hatua iliyofanya kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi