loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TIC  yaanza kukutanishwa na wawekezaji

SERIKALI imewahakikishia wawekezaji kuwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) imejipanga kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kuwaondolea vikwazo na changamoto zinazowakabili.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,  William ole Nasha katika kikao kazi kilichohusisha Menejimenti ya TIC pia wakurugenzi na wawakikishi wa wakurugenzi kutoka Bohari ya Dawa (MSD), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kikao hicho kililenga kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuweka mpango kazi ili kurahisisha uwekezaji thabiti na wenye tija kwa manufaa ya Watanzania. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Godius Kahyarara.

Aidha, alisisitiza kuwa wizara imejipanga kusimamia miradi yote ambayo imeanza kutekelezwa na serikali na taasisi ili kuhakikisha inaisha kwa wakati ikiwa ni moja ya maelekezo yaliyotolewa kwa wizara hiyo ambayo wanatakiwa kusimamiwa.

“Rais(Samia) katika hotuba zake amekuwa akisisitiza kwamba miradi ambayo serikali imeanza kutekeleza inapaswa kukamilika kwa wakati, tabia ya kuwa na miradi ambayo inaenda miaka na miaka bila kumalizika Rais(Samia) hataki ndio maana leo(jana) tumeanza utaratibu kama wizara iliyopewa jukumu la kuratibu uwekezaji nchini kujua miradi hiyo.

“Pia kuwa na kanzidata ya miradi yote ya uwekezaji pamoja na wawekezaji ili tuweze kufahamu na kusimamia, hii itasaidia kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ndio maana tumekutana na MSD, NSSF na NHC,”alisema.

Alisema wizara hiyo itaendelea kukutana na taasisi mbalimbali ili kuwaunganisha na TIC na kujadiliana kwa pamoja ni kwa namna gani wataweza kuboresha uwekezaji kwa kuzifahamu na kuzitatua changamoto mbalimbali kama ni za kisheria au kisera.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi