loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbeya zawapa wajasiriamali bil 3/-

SHILINGI 3,045,611,300 zilitolewa na halmashauri za wilaya zilizopo mkoani Mbeya kwa ajili ya mikopo ya kuviwezesha vikundi vya wanawake, vijana na walemavu kwa  mwaka wa fedha 2019/2020.

Fedha hizo ni  asilimia 10 ya mapato ya ndani ya kuviwezesha vikundi hivyo kuendesha miradi ya ujasiriamali.

Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 tayari halmashauri hizo zimekopesha makundi hayo jumla ya Sh 2,444,000,000 kwenye vikundi huku ukopeshaji ukiwa unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alibainisha hayo alipozungumzia hali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi hususani kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake na Vijana alipofanya mahojiano maalumu na HabariLEO.

Chalamila alisema mkoa kupitia halmashauri zake unaendelea kutekeleza mpango wa serikali wa kuyawezesha makundi ya wanawake, vijana na walemavu hususani waliojiunga kwenye vikundi vyenye lengo la kujitegemea na kujikwamua na umasikini kupitia shughuli mbalimbali halali.

Kwa mujibu wa Chalamila kwa mwaka wa fedha 2019/2020 vikundi 298 vya wanawake mkoani hapa vilipewa mikopo ya Sh 1,208,208,549,999, vikundi 210 vya vijana vikakopeshwa Sh 1,636,729,199 na vikundi 36 vya watu walio na ulemavu vikapewa jumla ya Sh 203,332,102.

Kwa mwaka wa fedha unaoendelea alisema katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana, halmashauri zimekopesha zaidi ya Sh bilioni 2.4 kwa jumla ya vikundi 386.

Kati ya fedha hizo vikundi 153 vya wanawake vilikopeshwa Sh 1,080,050,000, vikundi 96 vya vijana vikakopeshwa Sh 1,183,950,000 na vikundi 137 vya walemavu vikakopesha Sh 180,000,000.

Akizungumzia hali ya urejeshaji wa mikopo hiyo, Chalamila alisema jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha fedha zinazokopeshwa katika kila halmashauri kwa uwiano wa wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na walemavu asilimia mbili zinarejeshwa kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kuendelea kunufaika kupitia mpango huo.

Alisema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kiasi kilichorejeshwa kwenye mfuko ni Sh 1,356,621,608 na mwaka wa fedha 2020/2021 hadi Desemba mwaka jana zilirejeshwa kwenye mfuko Sh 1,103,090,091.

Akifafanua zaidi kwa upande wa walemavu, Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa una jumla ya watu wenye ulemavu 5,016 kati yao wanaume wakiwa 2,750 na wanawake 2,266 na kati ya hao wote watoto ni 1,270 huku watu wazima wakiwa 3,746.

"Jumla ya vikundi 63 vya watu wenye ulemavu vimeundwa katika Mkoa wa Mbeya, kati ya vikundi hivyo, jumla ya vikundi 43 sawa na asilimia 68.2 vimepata mkopo kutoka katika halmashauri zetu,"alisema.

Akizungumzia mikopo hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu nchini(Chawata) Jimmy Ambilikile ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mbeya aliipongeza na kuishukuru serikali kwa kulionaa kundi hilo kuwa lenye uhitaji wa kuwezesha ili liweze kufanya shughuli za ujasiriamali.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo,Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi