loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi akemea wanaume wanaotelekeza watoto

Zanzibar RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema si busara mwanamke kuachwa katika ndoa na kuachiwa watoto akihangaika nao bila ya kupewa msaada wa kukidhi maisha yake.

Alisema jana kuwa kuna umuhimu wa kurekebishwa sheria kandamizi ambazo zimekuwa zikiwakosesha wanawake haki za msingi visiwani Zanzibar.

Rais Dk Mwinyi aliyasema alipokutana na kuzungumza na viongozi wa Jumuiya ya Wanawake Wajane Zanzibar (ZAWIO), Ikulu Jijini Zanzibar.

Alisema ni vyema kwa jumuiya hiyo kuwa na mapendekezo yatakayosaidia kubadilisha sheria ili kuondoa upungufu wake na hivyo kuisaidia jamii .

Alisisitiza kwamba wapo wanawake ambao huchuma mali na wenza wao na mara wanapoachana hawaambulii chochote jambo ambalo alisema si busara licha ya baadhi ya wanaume kutoa visingizio vya kidini.

Dk Mwinyi alisema yuko tayari kutekeleza mabadiliko ya sheria ili sheria zisikandamize upande mmoja. Aliipongeza ZAWIO kwa kazi nzuri ya kujitolea kusaidia wajane Unguja na Pemba.

Alitoa Sh milioni 10 kwa ajili ya kuendesha ofisi ya jumuiya hiyo na vyakula vya futari kwa ajili ya wajane 300 wenye mazingira magumu zaidi.

Mkurugenzi Mkuu ZAWIO, Tabia Makame Mohamed alimpongeza Rais Dk Mwinyi kwa kuijali na kuiunga mkono jumuiya hiyo. Jumuiya hiyo ilianzishwa chini ya Sheria ya Asasi za Kiraia Zanzibar ya mwaka 1995, ikasajiliwa Desemba 12, 2019 na imejikita kuwasaidia wajane wa Zanzibar.

Tabia alisema Zanzibar hivi sasa ina jumla ya wajane 16,000 Unguja na Pemba.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu,

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi