loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndugulile ataja sababu vifurushi kwisha haraka

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema mifumo kwenye simu ni moja ya sababu zinayochangia vifurushi kwisha mapema.

Dk Ndugulile aliyasema hayo jijini Dodoma baada ya kikao cha robo tatu ya mwaka na taasisi zilizochini ya wizara hiyo kilichokuwa na lengo la kufanya mapitio ya mapato na matumizi kwa kila taasisi.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba vifurushi vinaisha kila baada ya muda.

Alisema, kuna visababishi vilivyomo kwenye simu ambazo wananchi wanazinunua ambavyo vinachangia tatizo hilo. “Kuna simu zingine zinafanya automatic updating (kuboresha mifumo yake ya uendeshaji), wakati mwingine inatumia data kwa hiyo kama hujaweka setting vizuri kila update inayokuja kwa kila application unayotumia inatumia data.”alisema Dk Ndugulile na kuongeza;

“Lakini wengine tunatumia mitandao ya whatsApp na kule hujaweka setting ya kuzuia picha zisijidownload (zisijifungue) kwa hiyo ukiwa na mitandao 100 au 1,000 na picha zote zinaingia kwenye simu yako zinatumia data.

Dk Ndugulile alisema, ni muhimu kwa taasisi zilizo chini ya wizara zikatoa elimu ya matumizi sahihi ya simu ili mtu asione kama ameibiwa kifurushi kumbe simu yake mwenyewe ndio inafanya kazi.

Alisema serikali inaweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha mawasiliano yanafika kwa wote, lakini bado kuna baadhi ya watu hawatumii inavyotakiwa na wanatakiw akuelimishwa.

Alizielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) kwenda kufanya ufuatiliaji wa malalamiko ili kuhakikisha kuwa kero za wananchi zinazohusiana na masuala ya mawasiliano yanashughulikiwa kwa wakati.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi