loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yafafanua tozo ya 1% kwa benki

SERIKALI imetoa ufafanuzi kuhusu tozo ya asilimia moja inayokatwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa ajili ya gharama za uchambuzi.
Akizungumza Bungeni leo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba alisema tozo hiyo ni gharama za uchambuzi wa maombi ya mkopo ambayo ni pamoja na shajala, uhakiki wa mradi na dhamana ya mkopo.

Dk Mwigulu aliyasema hayo akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee lenye vipengele (a) na (b)  na (c) aliyehoji Je ni nini sababu ya kuweka tozo ya ada ya tathmini ya asilimia moja kwa mkopaji ambapo asilimia 50 inalipwa kabla ya kuanza kufanya tathmini na asilimia 50 inalipwa baada ya mkopo kuidhinishwa;

“Ni kigezo gani kilipelekea tozo kuwa asilimia moja  na si vinginevyo na pia  mkopo usipoidhinishwa hiyo asilimia 50 ya asilimia 1 iliyolipwa inarudishwa?,”  alihoji Mdee.

Dk Mwigulu akijibu hilo alisema kigezo kinachotumika kutoza ada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ni gharama halisi za uchambuzi wa maombi ya mkopo zinazotokana na nguvu ya soko kwa wakati husika.

 Aidha, alisema utaratibu huo  ni wa kawaida kwa taasisi za fedha kutoza ada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo.

“Endapo mkopo hautaidhinishwa, asilimia 50 ya asilimia moja iliyolipwa hairejeshwi kwa mwombaji wa mkopo kwa kuwa kiasi hicho kimetumika kulipa gharama za uchambuzi wa mkopo,” alisema Dk Mwigulu.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi