loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Akaunti za Benki THRDC zafunguliwa

MTANDAO  wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema akaunti za benki za mtandao zilizofungwa kwa takribani miezi minane zimefunguliwa.

Taarifa ya Bodi ya  THRDC iliyosainiwa na Vicky Ntetema imesema kuwa kufunguliwa kwa akaunti hizo kumetokana na maelekezo kutoka kwa mamlaka ya serikali zilizoagiza kufungwa ili uchunguzi wa tuhuma  ufanyike na kisha kutoa maelekezo kwa benki kuwa zifunguliwe.

Tuhuma zilizokuwa zinakabili mtandao huo ni baada ya kitengo cha Polisi cha ufutatiliwa wa fedha haramu, kudai kuwa kimebaini kuna fedha nyingi zimeingia benki kwa kipindi cha Januari 2019 hadi Agosti mwaka 2020, Shilingi bilioni 6 zilidaiwa kuingia  kwenye akaunti za THRDC.

 “Kufungwa kwa akaunti hizo tangu Agosti 2020 hadi sasa, kulisababisha mtandao kushindwa kutekeleza sehemu kubwa ya majukumu yake kwenye miradi ya utetezi wa haki za binadamu kama ilivyokuwa imeainishwa kwenye mipango yake ya 2020,” imeeleza taarifa hiyo.

THRDC imetoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake unaojali na kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 21, 2021 na bodi ya mtandao huo na kutoa shukrani kwa wahisani, taasisi mbalimbali na wanachama walioshiriki kwa namna mbalimbali kuhakikisha mtandao unaendelea kutekeleza majukumu yake pia kuhakikisha kuwa changamoto husika zinatatuliwa.

Aidha  Bodi imewashukuru watendaji na wafanyakazi wote wa mtandao kwa kujitolea kuendelea na majukumu yao na uvumilivu waliouonyesha kipindi chote cha changamoto ya kutokuwepo kwa fedha za mtandao.

 “Bodi ya mtandao inapenda kuwashukuru wafadhili wa mtandao. Kwa kipekee, Bodi ya mtandao inamshukuru Rais Samia kwa uongozi wake unaojali na kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.

Ilisema mtandao huo  unaahidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na kwa kushirikiana na wadau na viongozi mbalimbali, mamlaka za Serikali, asasi za kiraia, mahakama, tume ya haki za binadamu, wadau wa maendeleo, vyombo vya habari, wanasheria, taasisi za kitaaluma, ofisi ya msajili wa asasi za kijamii na wanachama wake ili kuhakikisha kuwa utetezi wa haki za binadamu unafanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa hapa nchini.

Pia imeeleza kuwa mtandao utaendelea kufanya kazi bila hofu kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na taratibu zote zilizowekwa na mamlaka zote ikiwemo ofisi ya uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuendelea kudumisha na kuboresha ushirikiano katika kazi za utetezi wa haki za binadamu.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi