loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Ndaki: Fanyeni kazi kwa uadilifu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na uwajibikaji sambamba na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao.

Ndaki amebainisha hayo leo jijini Dodoma wakati akaifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo na kubainisha kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 “Niwaombe mjiepushe na vitendo vya rushwa haipendezi kuona mtumishi wa umma anatajwatajwa katika kashfa za rushwa, hili jambo sio jema hivyo hakikisheni mnaiepuka rushwa,” amesema Nadaki.

Katika hatua nyingine Ndaki amewahasa watumishi hao kuheshimiana pamoja na kuzingatia nidhamu ya kazi ikiwemo kujiepusha na vitendo vya ubabe na kudharauliana huku akibainisha kuwa kila mtu sehemu ya kazi ana umuhimu wake.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi