loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Balozi Mulamula aahidi kuimarisha uhusiano na Afrika Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini yameendelea kuimarika kutokana na historia iliyopo baina ya nchi hizo mbili tangu enzi za kupigania uhuru kwa nchi Kusini mwa Afrika.

Balozi Mulamula amesema hayo leo akiwa Petroria nchini Afrika Kusini alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Grace Naledi Pandor kujadili namna bora ya kuendeleza mashirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Katika mazungumzo yao Mawaziri hao wamejadili mchakato wa tathimini ya utekelezaji wa Bi-National Commission (BNC) ambapo kwa mwaka huu Afrika Kusini ndiyo itakuwa mwenyeji wa tathimini hiyo ambayo hujumuisha ngazi ya watedaji wakuu wa sekta mbalimbali wa nchi hizi mbili, mawaziri na huitimishwa na marais wa nchi zote mbili. 

Kwa upande wa Waziri, Grace Pandor amesema Taifa hilo linathamini mashirikiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili na kwamba kinachohitajika ni kuendelea kuimarisha mashirikiano ya kiuchumi na kisiasa. Amemshukuru Balozi Mulamula kwa kumtembelea nchini humo na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana  kikamilifu kujenga makumbusho ya urithi ‘heritage museum’ ya harakati za kupigania uhuru kusini mwa Afrika zenye chimbuko lake nchini Tanzania.

Aidha, Balozi Mulamula kabla ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, alikutana na watumishi wa ubalozi wa Tanzania Pretoria  na kupokea taarifa ya eneo la uwakilishi la Ubalozi ambalo linajumuisha Afrika Kusini, Botswana, Falme ya Lesotho na SADC. Taarifa hiyo ilieleza juhudi za Ubalozi katika kukuza mahusiano na nchi za eneo la uwakilishi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, diplomasia ya siasa, wanadiaspora wa eneo la uwakilishi.

Balozi Mulamula ameutaka Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kuendela kufanya kazi kwa malengo, watumishi kujiwekea malengo ili kufanikisha malengo ya Ubalozi na hatimaye Ubalozi kuchangia malengo ya Wizara kwa ujumla.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi