loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Urusi kufungua kituo cha kusaidia biashara Uganda  

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa Kiuchumi na Mataifa Kusini mwa Jangwa la Sahara (AfroCom), ina mpango wa kufungua kituo cha kusaidia biashara jijini Kampala nchini Uganda.

“Leo kwa mara ya kwanza tutatoa wasilisho la nyumba ya biashara ya AfroCom kama kituo cha msaada wa biashara cha Urusi jijini Kampala, Uganda,” alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Igor Morozov.

Alisema kupitia kituo hicho watafanya majaribio hasa jijini Kampala na kukifanya kituo hicho kuwa cha mfano katika masuala ya kibiashara.

“Tunataka kupitia kituo hiki kutoa uelewa wa namna ya kusaidia biashara baina ya Uganda na Urusi. Biashara ni zile za kati na ndogo, kutoka mikoa, ambayo iko tayari kuja Afrika na kufungua biashara, " alisema Morozov.

AfroCom ilianzishwa mwaka 2009. Kazi muhimu ya kamati hiyo ni kukuza masiahi ya biashara ya Urusi, Afrika.

KWA muda wa siku nne mfululizo, nchi ya India imeweka ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi