loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bilioni 14 kutumika ujenzi wa hospitali 28 mpya

SERIKALI imetenga shilingi bilioni 14 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya 28, ikiwepo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyotengewa shilingi milioni 500  kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo.
 
Hayo yameelezwa na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu,  wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Vijijini, Jonas Mbunda aliyehoji ni lini Serikali itaanza kujenga na kukarabati majengo ya hospitali ya wilaya hiyo kutokana na baadhi ya majengo kuchakaa.

Akijibu swali hilo, Ummy alisema “Serikali inatambua uchakavu wa baadhi ya Hospitali Kongwe za Halmashauri ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.”

“Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeona ni vema katika mwaka wa fedha 2021/22 kutenga na kuomba kuidhinishiwa bilioni 14 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali mpya 28 ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyotengewa milioni 500.

Alisema serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa kukarabati na kujenga hospitali mpya nchini, kwa awamu kadri ya upatikanaji wa fedha

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi