loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania yashiriki mkutano biashara, viwanda EAC

Tanzania yashiriki mkutano biashara, viwanda EAC

TANZANIA ni miongoni mwa nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizoshiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Waziri wanaosimamia sekta za biashara, viwanda, fedha na uwekezaji.

Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo, aliongoza ujumbe wa Tanzania ulioshiriki mkutano huo akiwa na Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukran Manya.

Ujumbe wa Tanzania pia ulijumuisha maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara; Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) na Wizara Madini. 

Mkutano huo iliofanyika juzi katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, ulilenga kujadili uendelezaji wa sekta ya viwanda katika EAC.

Utekelezaji wa ajenda hiyo unazingatia maelekezo yaliyotolewa na wakuu wa nchi EAC na Baraza la Mawaziri la Jumuiya kupitia mikutano iliyopita na pia kwa kuzingatia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja EAC. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zote sita wanachama EAC za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Sudan Kusini.

Jamhuri ya Kenya iliongoza mkutano huo na Katibu wa mkutano alitoka Burundi. 

Mkutano huo wa 37 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ulitanguliwa na mkutano ngazi ya watendaji wakuu EAC katika sekta hizo. Ulifanyika kwa njia ya mtandao Aprili 22, mwaka huu.

Aidha, mkutano wa ngazi ya wataalamu EAC mahsusi katika eneo la viwanda ulifanyika kwa siku mbili kwa njia ya mtandao Aprili 20 hadi 21 mwaka huu.

Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya wataalamu katika  mkutano huo uliongozwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na ulihudhuriwa na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda na Biashara, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Wataalamu wengine walitoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Madini, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),  Chama cha Wazalishaji Nguo na Bidhaa za Nguo Tanzania (TEGAMAT) na Mfamasia Mkuu wa Serikali. 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bec342214b2b28a341d2fc000b54dd3e.jpeg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi