loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kagame apongeza ugawaji chanjo za covid- 19

Kagame apongeza ugawaji chanjo za covid- 19

RAIS Paul Kagame ameridhishwa na kazi inayofanywa na programu ya kugawa na kusambaza chanjo ya covid- 19 (ACT) ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa huo.

Kiongozi huyo alisema hayo katika mkutano ulioendeshwa kwa njia ya video wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa utendaji kazi wa programu hiyo iliyoanzishwa mwaka jana kwa ajili ya kusaidia mataifa masikini kukabiliana na maambukizi ya corona.

ACT ilianzishwa Aprili, mwaka jana, ambapo imeiunganisha  dunia pamoja katika mapambano dhidi ya covid- 19. Progamu hiyo ilianzishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ushirikiano na wadau wake ili kujenga miundombinu ya pamoja ya kupambana na ugonjwa huo kwa kutengeneza na kuwezesha upatikanaji wa vipimo vya covid 19, matibabu na chanjo kwa wananchi. 

“Tutaendelea kufanya kazi pamoja na Shirika la Afya Duniani pamoja na washirika wengine ili kushinda vita dhidi ya covid 19,” alisema Rais Kagame wakati wa hotuba yake hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cf0fc4b3cddefb480dc7a580659a366a.jpeg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi