loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania, Rwanda zang’ara  utawala bora Afrika Mashariki

Tanzania, Rwanda zang’ara utawala bora Afrika Mashariki

RIPOTI ya Hali ya Utawala Bora na wa Sheria Afrika Mashariki imeonesha Rwanda na Tanzania zimefanya vizuri zaidi kuliko mataifa mengine katika jumuiya hiyo.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘Ripoti ya Usawa ya Dunia (WJP) 2020’ imeonesha kuwa, Rwanda ni ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki, huku ikishika nafasi ya 37 duniani kutokana na utawala bora na unaofata sheria.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania inafuata ikiwa nafasi ya 93 duniani, huku Kenya ikishika nafasi ya tatu Afrika Mashariki na nafasi ya 102 duniani. 

Ripoti hiyo imeonesha kuwa Uganda imechukua nafasi ya nne na ya 117 duniani.

Ripoti hiyo imesema jumla ya maraifa yaliyoshirikishwa duniani ni 128 ambayo yalipimwa kutokana na serikali zao zinavyoshughulikia changamoto za kiutawala pamoja na kufuata utawala wa sheria na utawala bora.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Rwanda imezipita nchi zilizokuwa na rikodi nzuri za utawala bora kama vile Mauritius ambayo imekuwa ya 43, Ugiriki ambayo imekuwa ya 45 na Afrika Kusini ambayo imeshika nafasi ya 58.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2cafa4b9001e4fcf06547b47de61599c.png

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi