loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Kiir aamuru ulinzi barabara kuu za kiuchumi

Rais Kiir aamuru ulinzi barabara kuu za kiuchumi

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa changamoto za usalama barabarani hususani mashambulizi na utekaji unaofanywa na vikundi vya waasi wanaojificha misituni katika Jimbo la Ikweta ya Kati kwa kuweka ulinzi mkali wa jeshi katika barabara zote kuu za kiuchumi.

Rais Salva Kiir ameliagiza jeshi kuweka ulinzi wa saa 24 katika barabara kuu za kiuchumi na zinazotumiwa kwa wingi na wananchi ili kuruhusu shughuli zifanyike bila usumbufu wowote.

Hayo yalisemwa na Gavana wa Ikweta ya Kati, Emmanuel Adil Anthony baada ya kumaliza kikao na Rais Kiir kalichofanyika Ikulu mjini Juba. 

Alisema katika mazungumzo yao, Rais Kiir alimthibitishia kuwa usalama wa barabara hizo utaimarishwa kwa gharama yoyote kwa sababu zinatengeneza uchumi wa nchi.

Maagizo hayo ya Rais Kiir yamekuja siku chache baada ya madereva nane kutoka Uganda na Kenya kuuawa katika  mashambulizi ya kushtukiza yanayoaminika kufanywa na kikundi cha waasi cha NAS, Machi mwaka huu.

“Ni jambo zuri sana kwa Rais Kiir kukubali kuongeza ulinzi katika barabara zetu kuu kuondoa vitisho vyote vya usalama hali itakayoruhusu biashara kuendelea na shughuli za kibinadamu katika jimbo zima na taifa kwa ujumla,” alisema Adil.

Alisema kutokana na changamoto za kiusalama katika eneo la mpaka, alitumwa na Rais Kiir kuzungumza na vyombo vya usalama vya Uganda na baada ya kurudi alimwelezea yale waliyokubaliwa katika kikao hicho, ingawa hakuyataja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0a9ea15af2cc87ef513de339b261ec36.jpeg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi