loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rodgers akataa mfupa uliomshinda Mourinho Tottenham

Kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers amesema hana mpango wa kuhamia Tottenham kuchukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kutimuliwa Kocha  Jose Mourinho.

Kwa mujibu wa mtandao wa SkySport, Rodgers anafikiriwa kuwa kwenye orodha ya wanaowania nafasi iliyoachwa na Mourinho, ambaye alipoteza kibarua Jumatatu iliyopita, zikiwa zimesalia siku sita kabla ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.

Mwingine aliyehusishwa na ukocha Spurs ni Kocha wa RB Leipzig, Julian Nagelsmann, lakini tayari ameshathibitishwa kuwa kocha mpya wa Bayern Munich kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Aidha, ripoti imesema Rodgers hana mpango wa kwenda Tottenham, na kuwa anayafurahia maisha kwenye klabu yake ya sasa, Leicester.

Katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, Leicester (nafasi ya tatu) ina jumla ya alama 62 ikiizidi alama tisa Tottenham (nafasi ya saba) yenye jumla ya alama 53.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: LEICESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi