loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasichana wahimizwa kujitambua wafanikiwe

VIJANA balehe hususani wasichana wametakiwa kujitambua na kujiamini ili kufikia ndoto zao kwa kuepukana vishawi vinavyoweza kuwatumbukiza katika maambukizi ya Ukimwi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dk John Jingu, alisema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana.

Dk Jingu alisema kujitambua na kujiamini ni nyezo muhimu kwa vijana ili kutimiza ndoto zao na pia, kupambana na changamoto za maisha zikiwemo za maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

"Naomba wasichana mjitambue na kujiamini kwani nyie ni nyenzo muhimu ya kutatua changamoto zinazoendana na umri wenu… Jiamini unaweza kupambana na changamoto, ukilegea kidogo ukiteleza utaharibu ramani ya maisha yako," alisema Jingu.

Alisema vijana balehe wakijitambua na kujiamini ipasavyo kwa mambo yenye tija kwao na kwa jamii, hawatabali kurubuniwa itakuwa rahisi na badala yake, watakataa vishawishi vinavyoweza kuwaangamiza kimaisha kwa kuharibu ndoto zao za kimaisha na kuwatumbukiza katika majanga mbalimbali yakiwamo ya mimba za utotoni na magonjwa ya zinaa ukiwamo Ukimwi.

Dk Jingu alivitaka vyuo na shule nchini kuanzisha madawati ya jinsia ili wanaopata changamoto na kufanyiwa vitendo vya ukatili waweze kufika kwenye madawati hayo na kupatiwa msaada.

Alisisitiza umuhimu wa nguzo kuu sita za Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya ya Maendeleo kwa Vijana Balehe ambazo ni kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa ijana, kutokomeza mimba katika umri mdogo, kuzuia ukatili wa kimwili na kisaiklojia na kuboresha lishe miongoni mwa vijana balehe.

Nguzo nyingine ni kuhakikisha watoto wanapelekwa shule na kumaliza masomo yao na kuwawezesha vijana balehe kupata fursa za kiuchumi kwa kuajiriwa na kujiajiri.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk Leonard Maboko, alisema nia ya Serikali ni kufikisha Afua za mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa kuwezesha vijana kupata fursa za mitaji na ajira ili kuondokana na changamoto za kukumbana na vishawishi.

  Alisema maabukizi ya Ukimwi kitaifa ni wastani wa asilimia 4.7 kiwango alichosema kitapungua kwa kuwalinda vijana walio katika umri hatarishi.

  "Asilimia 40 ya watu wenye maambukizi ya VVU ni vijana kati ya umri wa miaka 15 na 24 na asilimia 80 kati ya hao ni wasichana," alisema Dk Maboko

Mwakilishi wa wasichana balehe na wanawake vijana, Mariana Mathias kutoka Kyela mkoani Mbeya, aliishukuru Serikali na wadau kwa kuja na afua mbalimbali zinazolenga kuwasaidia wasichana balehe na wanawake vijana katika kupambana dhidi ya maambukizi ya VVU na Ukimwi kwani imewasaidia vijana wengi kujiamini na kujitambua.

 “Mimi ni mfano niliwezeshwa kutoa elimu ya fani ya urembo na kupewa vifaa wezeshi vinavyonisaidia kuendesha maisha yangu ya kila siku na hata kuendesha maisha ya familia yangu,” alisema Mariana.

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi