loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kwa wanaojua kuona, Rais ‘ameongeza mshahara’

JUZI Mei 1, Tanzania iliungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu, Mei Mosi iliyokuwa na kaulimbiu ya kitaifa: “Maslahi Bora, Mishahara Juu, Kazi Iendelee.”

Maadhimisho hayo yalifanyika kitaifa jijini Mwanza huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan yakiwa ni maadhimisho yake ya kwanza akiwa Rais baada ya kuapishwa Machi 19, 2021 kuiongoza Tanzania kutokana na kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli.

Mijadala mbalimbali ya watu baada ya maadhimisho hasa hotuba ya rais ambayo Watanzania wengi walikuwa wakiisubiri na sasa wanaendelea kuijadili inabainisha kuwa, kwa wanaojua ‘kuona’, ingawa rais hakutamka rasmi, kwa njia nyingine, Rais Samia ‘ameongeza mishahara’ hivyo, anastahili shukrani na pongezi maradufu.

Wanamshukuru na kumpongeza wakisema ingawa hakuongeza mishahara kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kiuchumi na kiafya kama kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Uviko maarufu Coviid-19 uliotikisa uzalishaji na masoko huku ukigharibu pesa nyingi kwa matibabu na kinga, Rais Samia amepunguza kodi katika mishahara maarufu PAYE kwa asilimia moja kutoka asilimia tisa hadi asilimia nane.

Hii ina maana kuwa, kiwango cha asilimia moja kilichokuwa kinaktwa kwenda kwenye kodi, sasa kitabaki katika mshahara wa mtumishi na kutoa huduma mbalimbali katika familia ndio maana ninasema: “Kwa anaojua kuona umuhimu na ukubwa wa hiyo asilimia moja, ni wazi wanajua Rais Samia ameongeza mashahara” hivyo, anastahili shukrani.

Kimsingi, Watanzania wamemwelewa vizuri Rais Samia kwa kuwaona, kusikiliza, kucheka nao na hata kulia pamoja ‘akivaa viatu’ vyao kimaisha ndio maana hata anapozungumzia changamoto za maisha ya Watanzania, anaonekana wazi alivyo na uchungu na Watanzania na alivyojitoa kuwasikiliza na kuwatumikia kwa upendo na dhati.

Mkuu wa Nchi Samia amezikonga nyoyo za Watanzania kwa kuahidi kuwa, endapo Mungu atapenda na mambo yakaenda vizuri zaidi, katika maadhimisho ya Mei Mosi, 2022, atatangaza nyongeza ya mshahara. Ahadi hii ni tumaini jipya na kubwa kwa watumishi na Watanzania kwa jumla.

Kubwa zaidi, Watanzania wanamshukuru kwa kuahidi kuendelea kutazama kwa makini makato yanayofanyika katika malipo ya mishahara ili yasiendelee ‘kuwaumiza’ watumishi na hivyo, ni anatarajia kufuta kodi na tozo zitokanazo na mishahara ambazo si rafiki kwa wafanyakazi. Hili nalo, linastahili pongezi na shukrani.

Kimsingi, Watanzania wanaojua kuona, wamefurahishwa na hatua za Rais Samia katika maeneo mbalimbali hasa aliposema ingawa mwaka huu imekuwa vigumu kwake kuongeza mishahara, serikiali itaendelea kuboresha zaidi mazingira na maslahi ya wafanyakazi katika kada mbalimbali nchini.

Kimsingi hata kitendo cha kuondoa asilimia sita ya malipo ya riba kwa wafanyakazi wanaofanya marejesho kwa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) baada ya kupata mikopo hiyo walipokuwa masomoni katika vyuo mbalimbali, kinaonesha kuwa Rais kwa namna isiyo rasmi, ameongeza mishahara kwa watumishi wengi wanaokatwa mishahara kulipa deni hilo kwa nyongeza ya riba.

Ndio maana ninasema, kwa wanaojuua kuona, Rais Samia Suluhu Hassan, ameongeza mishahara kwa watumishi. Anastahili pongezi, shukrani na kupewa ushirikiano zaidi.

LINUS Robert wa kijiji cha Mabamba, wilayani Kibondo, ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi