loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shehe apongeza CRDB kujali yatima Ramadhani

SHEHE wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuonesha upendo kwa yatima katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya benki hiyo kutoa futari katika vituo 40 vya watoto yatima vilivyopo maeneo mbalimbali nchini.

Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwahusisha waumini mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wafanyakazi pamoja na wateja wa benki hiyo.

ambapo pamoja na mambo mengine aliusia upendo kwa watoto yatima.

Shehe Alhad alisema kitendo cha benki hiyo kuwajali yatima kwa kuwapa futari kwa ajili ya kuwawezesha kufuturu ndani katika kipindi cha Ramadhani, kinaonesha upendo kwao na zaidi kinaendana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu ya kujali makundi mbalimbali yasiyo na uwezo hasa kipindi hiki ambacho kinamtaka kila muumini wa dini ya Kiislamu kufunga.

“Huu ni upendo ambao Mwenyezi Mungu amewataka watu wote waliojaliwa uwezo kujitoa kwa wale wasio nao, kwa hili ambalo CRDB mmelifanya mnastahili pongezi na niwaombe wengine kuiga mfano huu kwa kuwa mbali na kuwapa faraja walengwa nanyi mnapata baraka kutoka kwa Mungu,” alisema Shehe Alhad ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya amani Tanzania.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Amani, Mchungaji Geogre Fupe, alisema ni vyema kwa jamii kujenga utamaduni wa kuoneshana upendo wakati wote hata baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani na kwaresma ambao hivi karibuni waumini wa dini ya kikiristo wametoka kuutekeleza.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, mbali ya kuwashukuru viongozi hao na wengine wote kwa kukubali mwaliko wa futari hiyo, alisema wao wanajivunia upendo wanaoupata kutoka kwa watanzania wote.

Alisema kama siyo watanzania kwenda kupata huduma zao na benki hiyo wasingekuwepo na kusisitiza kuwa wao kama taasisi kubwa ya utoaji wa huduma za kifedha nchini, wanajivunia upendo wanaoupata kwa watanzania na kwamba hata msaada wanaoutoa kwa yatima umetolewa kwa ushiriki wa pamoja na wateja wao.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi