loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ummy: Marufuku kudai vyeti wanaoanza darasa la kwanza

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu amepiga marufuku kwa shule kudai cheti cha elimu ya awali kwa wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza.

Mwalimu alitoa marufuku hiyo bungeni leo wakati wa kujibu swali la msingi la  Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi (CCM).

Katika swali lake, Kisangi  alitaka kujua yapi majibu ya serikali kutokana na kuwepo kwa sharti la watoto wanaotaka kuandikishwa darasa la kwanza kutakiwa kuwa na cheti cha kuhitimu elimu ya awali hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akijibu swali hilo, Waziri Ummy amesema ni marufuku shule kudai certificate ya awali kwa wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza.

“Ninachotaka kusema, bado hatujafanya vizuri kuongeza access ya watoto kuanza elimu ya awali, kwa hiyo haileti mantiki kusema kila mtoto aanze darasa la kwanza awe na vyeti ya awali,” alisema Ummy

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi