loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Samia, Obasanjo wafanya mazungumzo Dodoma

RAIS Samia Suluhu Hassan mapema leo Mei 03, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo.

Katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema kuwa mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma ambapo Rais Mstaafu Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Hayati Benjamin William Mkapa na Hayati Dk  John Pombe Magufuli waliofariki dunia  Julai 23, 2020 na Machi 17, 2021 mtawalia.

Aidha Rais Mstaafu Obasanjo amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.

Katija mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.

Pia viongozi hao wamezungumzia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

 

 

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi