loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanadiplomasia: Rais Samia ameanza vizuri EAC

WANADIPLOMASIA wamesema Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu ameanza vizuri katika kuimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuanza na kutafuta suluhisho na nchi za jirani kabla hajaenda katika nchi nyingine.

Imeelezwa kuwa Rais amefanya hivyo kuhakikisha anaimarisha uhusiano wa kikanda ili kukuza uchumi wa nchi kwa kuangalia changamoto na fursa mbalimbali zilizopo.

Wameeleza hayo wakati leo Rais Samia anaanza ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo pamoja na masuala mengine, atahutubia Bunge la nchi hiyo na kukutana na kuzungunza na wafanyabiashara.

Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mbunda, alisema hatua hiyo ni mwanzo mzuri katika kuimarisha uhusiano na nchi jirani.

Mtaalamu wa Masuala ya Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam, Dk Wategere Kitojo, alisema jambo analofanya Rais Samia kwa sasa ni kukuza ushirikiano na uhusiano na nchi jirani kabla ya kuanza kukuza diplomasia ya uchumi.

Alisema diplomasia ya uchumi inayohusisha masuala mbalimbali ukiwemo utalii, biashara, uwekezaji na mengineyo inaweza kuimarika ikiwa kutakuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri.

“Kama ulivyoona, alianza na Uganda katika kutia saini mkataba wa bomba la mafuta; hii ni kukuza ushirikiano na sasa anaenda Kenya ambako ni mdau mkubwa wa biashara huku nchi hiyo ikiwa na uchumi mkubwa EAC ikifuatiwa na Tanzania, hivyo ni vema kuweka mambo sawa ili kuimarisha ushirikiano katika nyanja zote,” alisisitiza.

Rais Samia leo anafanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta.

Akiwa huko, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake kisha kuhutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha wabunge wa mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

Aidha, Rais Samia atahutubia Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika jijini Nairobi kujadili masuala mbalimbali yahusuyo fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania na Kenya.

Ziara hiyo ya ni ya pili kwa Rais Samia tangu aapishwe Machi 19 mwaka huu,kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, baada ya kufariki duania kwa Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli, Machi 17, 2020.

SERIKALI inakusudia kurejesha mfumo wa maendeleo ya sanaa ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi