loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha Yanga aipania Simba

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema baada ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, hawatakubali kupoteza michezo miwili mfululizo watakaposhuka Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuwakabili Simba, Mei 8.

Yanga inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 57, itashuka uwanjani katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Katika mchezo wa awali, bao la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalty baada ya Tuisila Kisinda kuchezewa vibaya na Joash Onyango, kabla ya beki huyo raia wa Kenya kusawazisha makosa na kuipatia timu yake bao la kusawazisha dakika za majeruhi na kuharibu sherehe ya Wananchi waliokuwa wakidhani mechi hiyo imeisha kwa timu yao kupata ushindi.

Akizungumza na HabariLEO, Nabi alisema anaifahamu vizuri Simba kwani amekutana nayo mara moja katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Al Merriekh ya Sudan.

Alisema Simba ni inafanya vizuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara, lakini hilo halitawazuia kufanya vema katika mchezo huo na kuondoka na pointi tatu.

“Baada ya kupata matokeo na kuingia hatua ya nane bora tunarudi kutafuta pointi tatu, najua utakuwa mchezo mgumu kwa upande wetu lakini naamini tunaenda kupata ushindi na kuondoka na pointi tatu,” alisema Nabi.

Alisema anaiheshimu Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wa daraja la juu lakini kwa maandalizi anayoendelea nayo anaamini wanaenda kuchukua pointi tatu na kupunguza idadi ya pointi na watani wao hao wa jadi ambao ndio vinara katika msimamo wa ligi.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi mwezi Januari na Yanga kuibuka kwa ushindi wa 4-3 kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 80 bila kufungana.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi