loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Meddie Kagere hesabu zote Yanga

MSHAMBULIAJI kiongozi wa Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere amesema wapo katika mipango imara kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Yanga ili kuongeza kasi ya kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne.

Mchezo huo umepangwa kupigwa Jumamosi, Mei 8 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mtanange huo wa kukata na shoka unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na malengo ya klabu hizo mbili ambazo ziko katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kagere ambaye hadi sasa amepachika mabao 10 anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji nyuma ya Prince Dube aliyepachika mabao 11 hadi sasa.

Akizungumza na HabariLEO, , Kagere alisema hivi sasa akili yake ipo katika mchezo dhidi ya Yanga ambao ni muhimu kwao katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, lakini pia ni wakati sahihi wa kupambana kuhakikisha anarejea kileleni na kumshusha Dube katika orodha ya wafungaji.

“Tuko vizuri na tunaendelea na mazoezi kwaajili ya mchezo ujao, nipo hapa kwaajili ya kuipambania timu yangu pamoja na kutimiza malengo yangu ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora ingawa najua msimu huu haitakuwa rahisi kutokana upinzani uliopo hivi sasa,” alisema Kagere.

Alisema lengo ni kuweka rekodi ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora kwa mara ya tatu mfululizo kama ilivyofanya timu yake kutwaa mataji ya ligi mara tatu mfululizo.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi