loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maandalizi Tulia Marathoni moto

MAANDALIZI ya msimu wa nne wa Mbeya Tulia Marathon 2021 utakaofanyika Jumamosi yamekamilika, imeelezwa.

Mbeya Tulia Marathon imekuwa ikifanyika kila mwaka na kushirikisha mbio za kilometa 42, kilometa 21, na mbio za uwanjani za meta 100, 200, 400, 800 na 1500.

Mbio hizo zina lengo la kuboresha miundo mbinu ya afya na elimu mkoani humo, na tayari zimesaidia shule na vituo kadhaa vya afya jijini Mbeya na Rungwe.

Akizungumza na gazeti hili jana, meneja wa Tulia Trust inayonadaa mbio hizo, Jaquline Boazi alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanariadha wanazidi kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio za umbali tofauti.

Boazi alisema kuwa mbio hizo zimekuwa zikisaidia kuboresha miundo mbinu mbalimbali katika hospitali na shule za mkoani Mbeya na tayari baadhi yake zimefaidika.

Akitolea mfano, Boazi alisema kuwa shule ya sekondari ya Roleza imefaidika kwa kufanyiwa ukarabati mabweni yake mawili la Azimio na Tulia, ambayo yalikuwa hayakaliwi kabisa na wanafunzi, lakini sasa ni miongoni mwa mabweni bora kabisa shuleni hapo.

Pia kuna hospitali ambazo zimefaidika baada ya kujengewa vyumba vya upasuaji na sehemu ya kubadilishia nguo madaktari na waaguzi.

Alisema washindi wa mbio zote wameandaliwa zawadi nono za fedha taslimu kwa wanaume na wanawake.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi